Rais wa Marekani, Donald Trump toka aingie madarakani amekuwa akisaini sheria mbali mbali ambazo zimekuwa zikibana baadhi ya nchi na wananchi wake kutokana na sheria hizo kuwa hasi.
Moja wapo ya sheria hizo ni ujengwaji wa ukuta kutenganisha nchi ya Mexico na Marekani ambapo amesema kuwa Serikali ya Mexico kugharamia ujenzi wa ukuta huo kitendo ambacho kimekosolewa vikali na rais wa Mexico, Enrique Pena Neto.
Mbali na hilo pia Trump atapatisha sheria ya nchi zenye waislamu wengi duniani raia wake kutoingia Marekani kuhofia usalama wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani.
Nchi hizo zenye waislamu wengi dunia ambazo raia wake hawatoingia Marekani kwa mujibu wa Trump nne kutoka bara la Asia na tatu kutoka Afrika.
Nchi hizo saba zilizokumbwa na katazo hilo ni Syria, Iran, Iraq, Yemen, Libya, Somali na Sudan hizo zote raia wake hawatoingia nchini Marekani labda rais Trumpa atakapomaliza utawala wake.