Mwaanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amekanusha kufungiwa kwa wimbo wake baada ya kuitwa ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Nay wa mitego anasema kuwa wimbo wake mpya haujafungiwa lakini kuna baadhi ya sehemu inabidi kurekebisha na kuutoa tena ukiwa hakuna baadhi ya vipande.

Nay wa mitego anasema kuwa “kikao kilikuwa ni kwa ajili ya wimbo wa alisema mabao haujafungiwa lakini siwezi kuongea mambo mengi sana kwa sababu kuna viongozi tulikuwa nao kwaio hao wataweza kuongea kile tulikuwa tunakiongea huko.”

Nay wa amesema kuwa kuteuliwa kwa baadhi ya wasanii kuwakilisha wasaii katika uongozi wa BASATA ni jambo zuri lakini hawezi kuliongelea kwaio bora wakae kimya waangalie jinsi wasanii hao pia watakavyoweza kufanya kazi.

Nay wa mitego alipoitwa na BASATA aliwahi kuposti picha ambayo ilileta wasiwasi kwa mashabiki wakidhani kuwa wimbo wake mpya umefungiwa katika vituo vya habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *