Mwanamuziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ameanzisha kampeni inayokwenda kwa jina la Nguvu ya Kitaa yenye dhamira ya kuwasaidia watu wenye hali za chini.
Kampeni hiyo itaanza rasmi kesho siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 14.
Nay amesema kuwa katika kampeni hiyo ambayo watatembelea Hospitali ya Tandale, nia ni kuwalipa fadhila watu wa kipato cha chini ambao wanafutilia kazi hizo lakini bado wanaishi katika mazingira magumu.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa anahitaji ushirikiano kutoka kwa wanahabari ili waweze kufanikisha jambo hilo kutokana na wasanii na vyombo vya habari kutegemeana.
Pia Ney amesema kuwa kutakuwa na matamsha ambayo watatembelea mikoa mbalimbali na wasanii ambao watatoa ushirikiano naye wakiwemo Young Killer Msodoki, Pam D, Chid Benz, Barnaba Classic, Msaga Sumu, Chemical, Qboy, Gigy Money na Mkali Wenu.
Kampeni hiyo itakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii ambao wamejitolea kushirikiana na Nay wa Mitego ili kuendeleza mshikamano na watu ambao wanafuatilia kazi za wasanii hata kama kipato chao cha chini.
Picha kwa hisani ya Global Publishers