Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amesema kuwa kafikirii Kuingia Kwenye Siasa Kabisa Kwasababu Atashindwa Kuwawakilisha Wananchi Vizuri Zaidi Kama Ambavyo Anawawakilisha Sasa Kupitia Muziki.

Nay wa Mitego amesema kuwa kwa upande wake yeye apendi siasa kwani anachofanya kwa upande wake anajisikia vizuri sana kuliko kuingia kwenye siasa ili kutafuta nafasi za uongozi.

“Mimi Sipendi Siasa Hichi Nachokifanya Najisikia Vizuri Zaidi,Nikiingia Kwenye Siasa Kuna Time Nitashindwa Kuzungumza Kwenye Interview Kama Hivi Kwasababu Utakuwa Umemuita Mwanasiasa Hivyo Tutazungumza Siasa” Amesema Nay wa Mitego

Pia Nay amesema kuwa Sasa Hivi anazungumzaa Matatizo Ya Watu Mtaani Tena Kwa Upana Zaidi Na Watu Wakanisikiliza Wengi Kuliko Watu Wakisema Huyu Ni Mbunge Wa Jimbo Flani Chama Flani Kuna Wakati Watanipuuzia.

Lakini Hivi Nawakilisha Kama Msanii Ambaye Nimeamua Kusimama Upande Wa Wananchi Ambao Wanapitia Changamoto Ambao Asilimia Kubwa Na Walala Hoi Wenzetu Na Ndio Wanaosapoti Muziki Wetu Na Ndio Wanaotafanya Tuishi Maisha Ambayo Tunaishi Kwahiyo Mimi Kuzungumza Matatizo Yao Ni Kujihusisha Nao” Aliongeza kwa kusema Nay.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *