Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa kwasasa anapeleka nyimbo zake BASATA kwa ukaguzi kabla ya kuziachia ili kuepuka kufungiwa.
Nay amesema kuwa kwasasa ameamua kufanya hivyo ili kuepuka migogoro baina yake na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na wizara ya habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Nay ni miongoni mwa wasanii waliokumbwa na rungu la BASATA baada ya nyimbo zake kufungiwa kutokana na kukosa maadili kwa jamii.
Pia Nay wa Mitego amesema kuwa licha kupeleka nyimbo zake Basata lakini bado msimamo wake ni uleule kuwa hawawezi kumpangia cha kuimba kwenye muziki wake.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii kufungiwa nyimbo zake na Nay wa mitego kuwa miongoni mwa waliofungiwa nyimbo zake.