Baada ya mkongwe wa hip hop Bongo, Profesa Jay kumrushia maneno makali Nash MC kuhusu tabia yake ya kuwaponda wana hip hop wenye mafanikio hatimaye Nash MC amemjibu mkongwe huyo.

Kupitia mtandao wake wa twitter Profesa Jay alimuelezea mwana hip hop kama mwenye wivu wa maendeleo kutokana natabi yake ya kukejeli harakati zinafanywa na wanamuziki wenzake wakati yeye mwenyewe hakufanya kitu kwenye muziki huo.

Nash MC kupitia mtandao akusita kujibu twet ya Profesa Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikimu mkoani Morogoro.

Mtu mwenye nidhamu ya uoga akiambiwa jambo huona anachukiwa.
Nidhamu ya uoga kwangu ilikaaga upande wa kushoto kitaaaaambo. Upumbavu Ni kipaji cha mtu haijalishi umri. Nna uhuru wa Kuongea nachotaka almuhimu nisivunje sheria za nchi,hakuna pimbi yoyote anaweza kunipangia swali la kuuliza kwenye muziki. Sijui utaenda nchi gani ukute hakuna Hip Hop. Hip Hop aihitaji Kuvuka boda. Ivuke boda iende wapi? Mbinguni? Unaimba kila aina ya muziki ili upate pesa sasa una tofauti gani na Malaya anaetembea na kila bwana apate pesa?? Mwanaume anatakiwa asimamie kila anachokiamini mpaka mwisho. Na ashinde katika imani yake.

Kutokana na majibizano hayo kunaonekana kabisa kuna tofauti kati ya wawili hao ambao wote ni wanamuziki wa hip hop Bongo huku Profesa Jay akimuacha kwa asilimia kubwa Nash MC kwa wasanii waliofanya mapinduzi ya hip hop hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *