Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemwagiza Mkurugenzi wa Habari Maelezo kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Nape amesema hayo wakati akizungumza na maofisa habari na mawasiliano wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika mkoani Dodoma.

Waziri huyo amesema kuwa “Nataka niiagize ofisi ya Mkurugenzi wa habari maelezo kuhakikisha kuwa mnafuatilia utendaji kazi wa kila ofisa habari na mawasiliano ili kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria au la na kama tutabaini kuna ofisa habari ambaye hatekelezi majukumu yake ipasavyo tumwombe atupishe.”

Pia waziri Nape ameongeza kwa kusema kuwa “Kutoa habari zinazohusiana na taasisi zenu mnazofanyia kazi ni jukumu lenu la kisheria na siyo hiari yenu kwa hiyo hakikisheni kuwa waandishi wa habari wanapowatafuta ili kupata habari kwenye ofisi zenu mnawapa taarifa sahihi na kwa wakati ili jamii iweze kupata”.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo hili kujiridhisha kama maofisa habari wanafanya kazi yao kwa ufasaha ili kufikisha habari kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *