Aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kupitia akaunti yake ya Instagram amelifananisha sakata la kutekwa kwa Roma na wenzake kama picha la kichina.
Nape ambaye ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi, kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka picha ya kipande cha gazeti chenye picha ya Roma huku akiandika maneno yaliosomeka ‘Da! Picha la kichina live!
Roma na wenzake jana walipatikana baada ya kutekwa siku ya Jumatano na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana wakiwa katika studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.