Aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo, Nape Nnauye ameeleza sababu ya kutembea juu ya migongo ya wananchi wa jimbo lake Mtama.

Nape ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi alifanyiwa na wapiga kura wake waliokitokeza katika mkutano wake alioufanya jimboni humo jumamosi iliyopita.

Mbunge huyo alipokewa kifalme kwenye jimbo lake na mpaka kusababisha kumwaga machozi wakati wa mkutano huo.

Nape alikuwa waziri wa Habari kabla hajaondolewa kwenye kiti hicho mwezi uliopita na Rais Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakembe.

Nape ametoa ufafanuzi huo kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima KIMILA na ukikataa ni sawa na DHARAU KUBWA kwa waliokufanyia, hata hivyo ndio maana NILILIZWA!.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *