Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo amefanya ziara ya kushtukiza kubaini wanaodurufu kazi za wasanii maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo waziri Nape ameongozana na maofisa wa TRA kwa ajili kuchukua maelezo kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo ya kudurufu kazi za wasanii ambapo ni kinyume na sheria.

nape

Waziri huyo pamoja na msafara wake wa operesheni hiyo wameingia baadhi ya maduka ya eneo hilo na kukagua kuhusu kujihusisha na biashara hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa waziri huyo kufanya ziara eneo hilo la Kariakoo ambapo mwaka jana alifanya ziara kama hiyo na kubaini wadurufu kazi za wasanii nchini.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *