Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameibuka na kudai kuwa alivunjika moyo kwa maneno ya udhalilishaji aliyoambiwa na msanii mwenzake Ray C baada ya kuimba nyimbo zake jukwaani.

Wiki chache zilizopita wasanii hawa wawili waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya  Nandy kutumia/ kuimba nyimbo za Ray C katika tamasha la Fiesta ambapo hakulipwa kwenda kuimba.

Ray C alimjia juu Nandy na kumwambia asitumie nyimbo zake kuingiza pesa kwani na yeye ni mwanamuziki hivyo anaweza kuimba nyimbo zake mwenyewe, jambo ambalo halikumpendeza Nandy ambaye alidai kuwa Ray C alikuwa na taarifa kuwa ataimba nyimbo zake kwani walikuwa wote THT kwenye mazoezi.

Nandy amesema kuwa maneno yale aliyoyaongea mtandaoni yalimdhalilisha sana kama msanii

Tangu ishu hii itokee Nandy amekuwa mtu wa kuizungumzia sana akionyesha kuwa hakufurahishwa hata kidogo tofauti na Ray C ambaye hajawahi kuongelea suala hili hata mara moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *