Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ametangaza ujio wa albam yake mpya na ya kwanza itwayo ‘The African Princess’, atakayoiachia rasmi Novemba 11 mwaka huu.
Nandy amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kupokea mzigo wa maana kutoka kwake, huku akiwapa njia ya kuweka oda (pre-order) mapema ili wawe wa kwanza kuipata.
Nandy unafuata nyayo za Vee Money alipokuwa akitoa Money Mondays mwishoni mwa mwaka jana, ambapo albam yake ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mauzo ya Boom Play Afrika Mashariki.
‘The African Princess’ pia inaweza kupata mapokeo ya maana lakini tu kama utambulisho wake utafuata njia nzuri na sahihi za kiubunifu kama ilivyokuwa kwa ‘Money Mondays’.
Kuna dalili nzuri pia kwa Nandy kwani ngoma ambazo tayari zimetoka ni kubwa tayari, tunasubiri zile ambazo zitaingia ndani ya albamu hiyo.