Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesikitika baada ya kusiki Rayvanny kulipishwa milioni 50 na WCB baada ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Nandy Festival.

Rayvanny Kutokea kama Surprise kwenye Tamasha la Nandy Festival Kule Songea na Kuzuka Stori Mitandaoni kuwa Lebo yake ya Zamani ya WCB imemuhitaji kulipa Kiasi cha Pesa cha Milioni 50 kwa kosa la Kukeuka Mikataba walioingia kwa kwenda kutumbuiza katika Tamasha hilo.

Sasa Mwenye Tamsha lake Nandy Amefunguka kwa Mara ya kwanza kuhusiana na hilo swala na Kusema kuwa Alijisikia vibaya baada ya kusikia Stori hizo japo kuwa hana uhakika nazo maana zimezuka tu Mitandaoni.

“Nimeziona hizo Taarifa na nimejisikia Vibaya maana nimeona kama mimi ndio niliosababisha hivyo Lakini niliona katika Instastory yake kuwa Ameandika yeye ni Msanii Huru hivyo Sikuamini kama Kalipishwa maana si unajua tena Stori za Mitandaoni”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *