Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy, amemshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pongezi alizompa, kwani ni kitu ambacho hakikutarajia.

Nandy amesema kuwa ni kitu cha faraja kuona anapongezwa na kiongozi mkubwa serikalini, hivyo kimempa faraja.

Kupitia akaunti yake ameandika “Nimefurahi kwa sababu ni mtu ambaye ananisapoti sana, na imenipa faraja sana kwani sikutarajia, kwa sababu mi nilitumiwa kwenye group nikaiona, basi nikampigia simu nikaongea naye nikamshukuru”.

Jana  Naibu Spika Tulia Ackson alipost kwenye instagram yake akimpongeza Nandy kwa jitihada zake anazozifanya kwenye kazi yake ya sana ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *