Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa anamshukuru mpenzi wake Billnass kwa kumvalisha pete ya uchumba.
Nandy ni mchumba wa Billnass ambaye wamekuwa wakipita kwenye vipindi vya kupanda na kushuka kwa penzi lao.
Wikiendi iliyopita Nandy alivunja ukimya baada ya kumshukuru Nenga na kusema kuwa, Jumapili iliyopita ilikuwa ni siku kubwa kwao huku wengi wakiamini labda walikuwa wanafunga ndoa.
Nandy ameandika kuwa ‘Asante kwa kunichagua tarehe 20/2/2022 ni siku special kwetu sisi wawili’ aliandika Nandy
Hata hivyo, kwa siku za hivi karibuni penzi lao limenoga kiasi cha kupewa majina tofauti na mashabiki kutokana na kuipenda kapo yao.