Msanii wa muziki wa Bongofleva, Nandy amevunja ukimya kuhusu tetesi za kuachana na mpenzi wake mwanamuziki mwenzake, Bilnass.

Ukimya huo kauvunja alipokuwa akizindua msimu wa pili wa tamasha lake la Nandy Festival litalotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.

Nandy amesema maneno yanayosemwa kuhusu kuachana na mpenzi wake huyo watu wayapuuze kwani hakuna mahali wenyewe wameshatoka mbele na kusema wameachana.

Wakati kuhusu ushiriki wake kwenye Nandy Festival inayoanza kurindima Juni 6 mkoani Kigoma, amesema Billnas atakuwepo kwani ni moja ya watu ambao tamasha hilo linamuhitaji.

Amesema jumla ya mikoa saba tamasha hilo litarindima huku Mkoa wa Kigoma ukiwa wa kwanza kufungua, na mikoa miwili itakuwa ya Kenya ambayo ni Nairobi na Mombasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *