Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa mwaka 2021 umekuwa mwaka wa baraka sana kwake toka aanze kazi yake ya muziki.

Nandy ameandika kuwa ni miaka sita sasa mmekuwa na mimi bila kunichoka tazama tunaingia mwaka wa 7 kwa kishindo!

Bila MUNGU bila nguvu zenu isingewezekana! Tumefanya mengi matukio makubwa ambayo hata mimi nikikaa mwenyewe nawaza nimevukaje hapa! Ila kwa support yenu tumeweza!

2022 najua kila mtu ana wish uwe mwaka mzuri ila pia tusisahau sisi tunapanga na MUNGU naye anapanga na MAADUI Nao wanapanga kikubwa dua MUNGU atasimama kama alivo simama mwaka huu!

Niombe radhi kwa yoyote niliye mkwaza mwaka huu na me nimesamahe wote kwani wenye mioyo safi huishi kwa amani.

Asanteni kwa kunifanya mwanamke wa mfano role model wa wengi niahidi hii nguvu ya mwaka huu ni juu yenu mwakani tunayo mengi IN GOD WE TRUST NAWAPENDA HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *