Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa kama msanii mwenzake, Dogo Janja angemuoa Irene Uwoya ni lazima angealikwa kutokana na ukaribu waliokuwa nao.
Nandy amesema kipindi hiyo ishu inatokea alikuwa kwenye ziara ya kimuziki lakini licha ya hivyo ni wazi angejulishwa.
Amesema kuwa “Kwa kuwa ishu imebainika ni kiki sioni haja ya kuwalaumu wawili hao kwa kuwa naamini hawakukurupuka kufanya hivyo. Lakini kama ingekuwa kweli ningealikwa tu,”.
Hivi karibuni kuliibuka taarifa kuwa Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa wiki iliyopita jambo ambalo lililozua utata kwa baadhi ya mashabiki wa wawili hao.
Harusi hiyo ilihudhuliwa na baadhi ya mastaa nchini kama vile Madee, Babu Tale, Tunda Man pamoja na Kassim Mganga.