Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameamua kwenda Basata kuomba msamaha baada ya video yake ya nusu utupu akiwa na Bilnass kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Nandy amemua kujisalimisha mwenyewe katika ofisi hizo ili kuepuka lungu la taasisi hiyo inayosimamia Sanaa nchini.
Jana katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ya nusu utupu ikimuonesha Nandy akiwa na Bilnass mpaka kupelekea watu kuhoji kwanini wameamua kurusha video hiyo katika mitandao ya kijamii.
Akiwa katika Baraza hilo Nandy ameomba radhi na kujutia kosa lake alilofanya na kuahidi kutorudia tena.
Pia kupitia akaunti yake ya Instagram, Nandy amewaomba radhi mashabiki wake waliokwazika kutoka na kusambaa kwa video hiyo.