Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameachia EP yaje ya nyimbo za dini inayokwenda kwa jina la ‘Wanibariki’  ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tofauti na alivyozoeleka akiimba za kidunia.

EP hiyo ya Nandy imebeba  nyimbo tano ambazo ni ‘Wanibariki’, ‘Umenifaa’, ‘Nipo Naye’, ‘Asante’ na ‘Noel Song’.

Nandy amesema alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye nyimbo za dini, amefurahi kuona ametimiza ndoto yake kutokana na kuwa shabiki mkubwa wa nyimbo hizo tangu akiwa mtoto.

“Nimelelewa kanisani, nyimbo za dini zipo kwenye maisha yangu na ndio maana nimekuwa nikiiziimba zinazoimbwa na waimbaji wa injili, ninafuraha iliyopitiliza kutimiza ndoto yangu, wanaotaka kuzisikiliza basi watazikuta kwenye EP yangu, watabarikiwa sana,”amesema  na ameongeza kuwa;

‘Wanibariki EP’ imetayarishwa kwenye studio za Wanene kwa ushirikiano wa karibu na kampuni ya Boomplay na Nandy mwenyewe, hivyo naamini wapenzi wa muziki wangu watafurahia kuniona kwa ujio huo mwingine,”amesema.

Nandy amewahi kufanya ‘cover’ za nyimbo za dini za waimbaji kama Joel Lwaga (Mimi Ni Wa Juu) pamoja na Angel Benard (Nikumbushe Wema Wako).

Katika upande wa Bongo Fleva msanii huyu hivi karibuni ameachia ngoma yake na msanii mkongwe kutoka Dr Congo, Koffie Olomide inayokwenda kwa jina la Leo leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *