Waziri wa michezo nchini Kenya, Hassan Wario ameivunja Kamati ya Taifa ya Olimpiki kuhusiana na maandalizi ya timu hiyo kwa michezo ya Olimpiki iliyomalizika Rio de Janeiro nchini Brazil.

Waziri huyo ametangaza hatua hiyo kwenye kikao na waandishi wa habari nchini ikibainika kwamba bado kuna wachezaji ambao hawajaondoka Rio mpaka sasa.

Wachezaji ambao bado hawajarudi Kenya kutoka Rio ni mbunge, Wesley Korir aliyeshiriki mbio za Marathon ambaye amesema wanaishi katika hali duni nchini Brazil.

Waziri Wario amesema majukumu ya kamati hiyo maarufu kama NOCK yatatekelezwa na Sports Kenya kuanzia leo.

Waziri huyo pia ameunda kamati ya kuchunguza yaliyojiri wakati wa maandalizi ya michezo hiyo na wakati wa michezo yenyewe iliyomalizika nchini Brazil.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *