Muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf ametangaza rasmi kuachana na muziki huo na badala yake atageukia katika kumrudia Mungu kwa kufanya ibada zaidi.

Mzee Yusuf amesema ameamua kupumzika kuimba muziki hili kuwaachia wasanii wachanga waweze kuendeleza fani hiyo kwani yeye alipofikia panatosha na kama kusaidia fani hiyo ameseaidia sana kwani kila pembe ya nchi muziki huo unajulikana.

Vile vile ameongeza kwa kusema licha ya yeye kuamua kuachana na kuimba lakini bendi yake ya Jahazi Modern Taarab itakuwa inafanya kazi kama kawaida chini ya mke wake Leila Rashid.

 Mzee yufuf ni miongoni mwa waimbaji wa muziki wa Taarab waliousaidia muziki huo kujulikana zaidi ambapo nyimbo zake zilikonga nyoyo za watu kufikia kupata umaarufu nchi nzima pamoja na baadhi ya nchi za nje kama Kenya na Uganda.

Mzee: akiimba kwenye moja ya show zake akiwa na bendi yake ya Jahazi Modern Taarab.
Mzee Yusuf: akiimba kwenye moja ya show zake akiwa na bendi ya Jahazi Modern Taarab.

Muimbaji huyo ni mmiliki wa kundi la Jahazi Modern Taarab ambalo limejizoelea umaarufu mkubwa kwa kuwa miongoni mwa makundi bora ya Taarab kuwahi kutokea nchini ambapo kupitia kundi hilo wasanii kibao walipitia na kujulikana kama vile Isha Mashauzi, Mariam Mcharuko, Khadija Yusuf, Amigo, Leila Rashid, Mariamu Amour na wengine kibao.

Mzee yusuf pia aliwahi kupitia makundi mengine kabla ya kuanzisha bendi yake ya Jahazi Modern Taarab ambapo aliwahi kuimba katika bendi ya East Afrika Melody na Zanzibar Stars Modern Taarab.

Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu mzee yusuf ni Msumali, Daktari wa Mapenzi, V.I.P na nyingine kibao zilizowahi kutamba katika anga ya muziki wa taaarab nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *