Mwanamuziki wa Taarab, Mzee Yusuf amefunguka na kusema kuwa, watu wanaomsema kuwa amerudi mjinilakini hashtui, ni wale ambao mashabiki wake wa kweli.
Mzee Yusuf kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Nimerudi Town anasema kuwa, asilimia kubwa ya watu wanaoongea kuhusu kufeli kwake baada ya kutangaza kurudi mjini.
Amesema kuwa siyo mashabiki wake kindakindaki na wala huwa hawafuatilii shoo zake kwa sababu kama wangekuwa wanafanya hivyo wasingekuwa wanaongeaongea.
“Wanasema nimerudi mjini sishtui? Unajua hao watu wanaokesha kunisema kuwa kwa sasa sishtui, mimi wala siwashangai kwa sababu naamini kabisa siyo mashabiki wangu na wala kwenye shoo zangu huwa hawahudhurii kabisa ndio maana wanakuwa na maneno mengi,
Pia amesema kuwa laiti kama wangekuwa wananifuatilia vizuri, basi wangegundua kuwa mimi ndiye msanii pekee wa Taarab kwa sasa ambaye ninajaza kwenye shoo zangu, sasa sijui wanataka nirudi vipi mjini.