Mzazi mwenzie na msanii Alikiba Devotha ambaye amezaa naye mtoto wa kiume anayefahamika kama Kiba Junior amesema kuwa atahudhuria kwenye harusi ya mwanamuziki huyo.

Mwanamke amesema kuwa yeye atahudhuria katika harusi hiyo ila anakwenda kama mama wa Alikiba na kudai kuwa msanii huyo amekuwa baba bora siku zote na kumtakia aendele hivyo hivyo hata baada ya kuoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanamke ameandika “Leo ni siku yako maalum Kiande wangu, rafiki yangu na baba bora Alikiba, baba usiniangushe somo yako. Mungu akusimamie katika ndoa yako. Mimi leo naenda kama Mama K, ukawe mume bora na ujali familia zote, nenda mwanangu”.

Ndoa ya msanii Alikiba inafanyika nchini Kenya katika mji wa Mombasa leo April 19, 2018 ambapo msanii huyo atachukua jiko lakini pia inategemewa kufanyika sherehe nyingine nchini Tanzania siku za karibuni ndani ya mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *