Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amesema amefurahishwa na utenda kazi wa Rais John Pombe Magufuli katika kipindi cha mwaka mmoja toka achukue madaraka.

Mwinyi amesema kiongozi huyo kwa sasa amepiga hatua sana katika kupambana na rushwa katika sekta za umma nchini na kusababisha wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma.

Rais huyo mstaafu ameyasema hayo wakati alipomtembelea Rais huyo Ikulu jijini Dar es Salaam na kubainisha kwamba anafurahishwa na utendaji wa Rais Magufuli kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kuweza kubana matumizi.

Pia Mwinyi amesema kiongozi huyo amepiga hatua sana pia katika kuimarisha utendaji kazi Serikalini.

Mzee Mwinyi mwenye miaka 91 alianza kuongoza Tanzania baada ya kupokea madaraka kutoka kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia mwaka 1985 hadi1995 na yeye kumuachia madaraka Benjamini William Mkapa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *