Baada ya msanii wa hip hop Roma Mkatolikia kukamatwa akiwa na wenzake katika studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini atoa agizo kwa polisi kufuatilia jambo hilo.
Roma na wenzake walikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.
Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la kutekwa kwa wasanii hao.
“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”.