Mwanansheria wa upande wa upinzani wa Kenya,Miguna Miguna amekataliwa kuingia Kenya baada ya kukataa kuomba Visa.

Bwana Miguna anasafiri kwa kutumia kibali chake cha kusafiria cha Canada baada ya kuvuliwa uraia wa Kenya.

Mamlaka ya Kenya ilimrudisha Canada baada ya kushiriki katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama “Rais wa watu”.

Wiki iliyopita Miguna aliiambia BBC kuwa mamlaka ya Kenya haijafuata maagizo ya mahakama ya kumpatia hati za kusafiria za Kenya.

Serikali ya Kenya ilimvua uraia Miguna na kumrudisha Canada ambapo pia ni raia huko.

Mahakama ya kenya ilitoa amri kwa serikali hiyo kurudisha hati za kusafiria za Miguna na kusaidia katika kurejea kwake lakini kwa mujibu wa Miguna serikali haija fanya hivyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *