Mwanariadha wa Urusi, Mariya Savinova amepokonywa medali yake ya dhahabu aliyoshinda kwenye mashindano ya London mwaka 2012 baada ya kubainika kuwa ametumia dawa za kusisimua misuli.

Mariya Savinova alishinda medali hiyo ya dhahabu mwaka 2012 katika mbio za mita 800 zilizofanyika Jijini London nchini Uingreza mwaka 2012.

Kutokana na kupatikana na kosa hilo la kutumia dawa za kusisimua misuli mwanariadha huyo amepigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya mbio mpaka mwa 2019 baada ya adhabu yake kumalizika.

Vile vile matokeo yote ya mbio za mwanariadha huyo tangu Julai 2010 hadi Agosti 2013, yamefutwa baada ya kupatikana na kosa hilo..

Katika mbio za London Savinova alimshinda mwanariadha kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya na pia mbio za dunia za riadha mwaka 2011 huko Daegu, Korea Kusini.

Mwanariadha huyo huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alimshinda Muingereza Jenny Meadows katika mbio za mataifa ya Bara Ulaya mwaka 2010 na kumfanya kunyakua medali ya shaba. Sasa medali zote za wanariadha hao wawili Jenny Meadows na Caster Semenya zitaborudishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *