Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Simbu amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza na kushinda mbio ndefu kwa wanaume (marathon) za msimu wa 14 zilizofanyika jana Mumbai nchini India.
Simbu alifanikiwa kuzishinda changamoto kutoka kwa mshindi wa pili Joshua Kipkorir wa Kenya ambaye alikuwa anamfuata nyuma kwa muda mrefu.
Simbu alimaliza mbio hizo za kilimita 42.195 kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 32 ambapo Kipkorir alikuwa wa pili kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 50.
Baada ya kushinda mbio hizo mwanariadha huyo amesema kuwa mbio hizo zilikuwa ngumu kutokana na washiriki kujipanga zaidi lakini anashukuru mungu.
Ushindi wa wanaume na muda waliotumia
1 Alphonce Simbu (TANZANIA) 02:09.32
2 Joshua Kipkorir (KENYA) 02:09.50
3 Eliud Barngetuny (KENYA) 02:10.39