Mwanariadha wa Kenya, Charles Maroa amefariki dunia kwenye hospitali ya KCMC iliyopo Moshi baada ya kuanguka wakati akishiriki mbio za Kili Marathon zilizofanyika jana mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa amethibitisha kutokea kifo hicho kwa kusema kuwa mwanariadha huyo amekutwa na umauti majira ya saa tano asubuhi katika hospitali ya KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.

Mwanariadha huyo alianguka getini wakati akikaribia kumalizia mbio hizo zilizofanyika jana na kushirikisha wanariadha mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kila mwaka ufanyika mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kuanguka alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini alipofika hospitali majaira ya saa tano asubuhi akafariki dunia.

Mashindano hayo yalianza majira ya Asubuhi na kumalizika majira ya jioni ambapo wanamuziki Joh Makini na Dogo Janja walipata nafasi ya kutoka burudani kwenye mashindano hayo ya riadha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *