Mahakama kuu ya rufaa nchini Afrika Kusini imemuongeza adhabu ya kukaa jela mwanariadha na mshindi wa Olimpiki Oscar Pistoius kutoka miaka 6 hadi 13 kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Hukumu iliyotolewa na mahakama asubuhi hii mjini Bloemfontein imebatilisha kutoka kifungo cha miaka 6 jela alichokuwa amepewa awali mwanariadha Oscar Pistorius hadi kifungo cha miaka 13 na miezi 5 jela.

Jaji wa mahakama hiyo ya rufaa Willie Seriti amesema kwamba Pistorius ilibidi ahukumiwe jela miaka 15 lakini mahakama imeangalia muda ambao tayari ameshakaa jela hivyo kumpunguzia hadi miaka 13.

Oscar Pistorius ambaye ni mlemavu wa miguu, alipatikana na hatia ya kumuua kwa kumpiga na risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp kwenye siku ya wapendanao mwaka 2013.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *