Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nini amekanusha kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego.
Nini amesema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Nay wa Mitego isipokuwa ukaribu wa kikazi tu.
Mwanamuziki huyo amefunguka hayo baada ya taarifa kusambaa kuwa amefukuzwa kwenye lebo ya MJ Records chini ya producer Daxo Chali kwasababu ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Nay wa Mitego.
Pia Nini ameongeza kwa kusema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Nay wa Mitego isipokuwa na mahusiano ya kikazi tu.
Ameongeza kwa kusema kuwa afikirii kama mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuathiri muziki wake.
Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo ‘Niwe Dawa’ aliyoshirikiana na Nay wa Mitengo ambayo inafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya Radio na Tv nchini.