Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amefanikiwa kujifungua mapacha -mvulana na msichana katika eneo la Burgos, kaskazini mwa Uhispania.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa amefanyiwa matibabu ya uzazi nchini Marekani kulingana na vyombo vya habari vya Uhispania.
Mwaka 2012 mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike ambaye baadaye alichukuliwa na kulewa na huduma za kijamii licha ya wasiwasi kuhusu hali yake.
Wafanyikazi wa kijamii wamesema kuwa msichana huyo alilewa akiwa pekee ,akiwa na mavazi mabaya mbali na uchafu wa eneo alilokuwa.
Hakuna uamuzi uliochukuliwa kufikia sasa kuhusu mama ya mtoto huyo.
Yeye na mamake wanadaiwa kuwa katika afya nzuri hospitalini. Mvulana huyo ana uzito wa kilo 2.4 huku msichana akiwa na uzito wa kilo 2.2.