Mwanamke mmoja amejifungua mtoto wa kike ndani ya ndege ya shirika la ndege la Uturuki wakiwa angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800.
Abiria walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso.
Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.
Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini wakati aliposhikwa na uchungu wa kujifungua.
Mashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.