Idara ya Habari Maelezo imetoa masaa 24 kwa Gazeti la MwanaHALISI kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kutokana na kuchapisha habari yenye kichwa cha habari cha kumchafua rais.

Gazeti hilo linalotolewa na kampuni ya Hali Halisi jana lilichapisha kichwa cha habbari kilichosomeka “Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM.

Taarifa ya Idara ya Habari Maelezo iliyotolewa jana imesema habari hiyo iliyochapishwa katika toleo la Jumatatu, Januari 30-Februari 5, 2017, inajenga dhana kuwa Rais Magufuli anahusika na kilichoitwa ufisadi wakati msingi wa taarifa husika ni tatizo la manunuzi katika Shirika la Elimu Kibaha!

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi awa Maelezo, Hassan Abbas, ilisema katika siku za karibuni Serikali imejitahidi kufanya mazungumzo na wahariri wa gazeti hilo kwa lengo la kukumbushana maadili ya uandishi wa habari, lakini “bahati mbaya kwamba wamekuwa wakikaidi japo wito tu”.

Ilisema kuwa iwapo wahusika wataona muhali kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na masharti ya usajili ya gazeti husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *