Mwanafunzi wa Luck Vicent, Doreen aliyoko Marekani kwa matibabu amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.

Madaktari waliowezesha upasuaji huo wamesema kuwa upasuaji umefanikiwa kwa ufanisi kupita matarajio yao.

Mwanafunzi huyo alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadrio ya masaa 5:30 lakini lakini zoezi hilo lilikamilika kwa muda wa masaa 4:00.

Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupekewa ICU, na Madaktari wamesema kwakuwa  hali yake imeridhisha sana kwa hiyo leo wanatamtoa ICU ambapo wamempunzisha baada ya upasuaji na kumpeleka wodi ya watoto.

Mwanafunzi huo ni miongoni mwa wanafunzi watatu waliosafirishwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya gari wilayani Karatu Mkoani Kilimanjaro na kusababisha vifo vya wanafunzi 32 na walimu wao wawili na dereva wa gari hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *