Mwamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amefunguka na kusema kuwa kuna wakati alipata changamoto katika muziki na kumfanya akate tamaa na kutaka kuacha muziki ili aende kuajiriwa sehmu nyingine.
Mwana Fa amesema kuwa pamoja na kwamba alikuatana na changamoto za kumkatisha tamaa lakini aliona sio vyema kuacha kazi ya muziki na kwenda kuajiriwa ingawa akitaka kwenda kuajiriwa anaweza kuapata kazi muda wowote.
Pia Mwana Fa anasema kuwa katika kila kazi hakuna sehemu yenye urahisi wa kila kitu kwaio hata kama angeacha kazi ya uziki na kwenda kuajiriwa hasingekuta kuwa huko ndio kuna mambo rahisi sana,maana hakuna sehem iliyotambarare tu , hivyo kitu cha kufanya ni kujikaza na kufanya kazi kwa moya na kujituma bila kukata tamaa na hili amewashauri hata wasanii wengine.
Mwana Fa ni moja kati ya wasanii wachache wasomi wenye kujivunia muziki wao pamoja na elimu kubwa walionayo, hivyo ukiachana na kazi ya muziki lakini pia ni msanii msomi mwenye uwezo wa kuajiriwa kokote kulingana na elimu yake.
Wapo baadhi ya wasanii wamekuwa wakitokomea kusiko julikana na kuacha kazi ya muziki kwa sababu ya mambo magumu wanayokuwa wanakutana nayo katika tasnia.