Mkali wa hip hop Bongo, Mwana FA amefunguka kwa kusema kuwa muziki wake hauna soko kubwa nje ya nchi hivyo hawezi kutumia nguvu nyingi kutafuta wasanii wa kimataifa kufanya nao kolabo.
Mwana FA amedai kwamba lengo la muziki wake ni kuwafikia watanzania wote na kuwaburudisha vizuri maana ndio watu ambao anaamini wanaushabikia sana muziki kuliko nje ya nchi.
Muimbaji huyo wa Dume Suruali amesema kuwa “Aina yangu ya muziki ni kuanzia maneno na lugha yangu ni kuwafikia watu wote wale waliopo ofisini na tai zao hadi mama Tatu aliyeko Tandika na sinia lake la vitumbua.
Pia amesema kuwa sina mahali ambapo ninaacha lakini ni hapa hapa nyumbani kwa sababu nachokiimba kina-relate na maisha yetu ya kila siku kwa upande wangu naona soko langu halipo nje ya nchi”.
Vile vile ameongeza kwa kusema kuwa “Wale ambao wameshafanya kazi na watu wa nje hawajakosea kwani naamini watakuwa wamejiongezea mashabiki wa nchi zingine, Good Luck to them lakini pia wanaendelea kujitengenezea ‘Cv’ nzuri…. Lakini kwa upande wangu sijawahi kufikiria au kuweka nguvu yoyote ya kuweza kuwapata wasanii wa kimataifa, kwani hapa ndani wasanii wapo wengi na sidhani kana nitaweza kuwamaliza”.
Pia Mwana FA amethibitisha kuwa mpaka sasa ana kolabo tisa ambazo anataraji kuzifanya huku nyingine zikiwa tayari kuachiwa kwa mashabiki.