Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mwakyembe amefunguka na kusema serikali itaendelea kuboresha Sheria, kanuni pamoja na kushirikiana na bodi ya filamu kuandaa mikataba bora itakayoongoza tasnia ya filamu kuwa na mafanikio makubwa.

Waziri Mwakyembe amewataka Watanzania kiujumla kupenda kazi za wasanii wa filamu za ndani ya nchi ili kuwaunga mkono wasanii wa ndani kwa kazi zao wanazofanya ambazo zinaonyesha uhalisia wa maisha ya Kitanzania.

Mwakyembe amesema kuwa “Tasnia ya filamu nchini inakua, watanzania tupieni jicho kwenye filamu za bongo kuwaunga mkono vijana wengi wanaotumia tasnia hiyo kuonyesha uhalisia wa maisha mbalimbali yaliyomo ndani ya jamii zinazotuzunguka”.

Wasanii wa filamu nchini wamekuwa wakilalamika kuhusu usambazaji wa kazi zao huku baadhi ya wasambazaji wa kazi hizo wakisema kuwa kumekuwa na changamoto ya soko kutokana na kazi hizo kunyonywa na kuuzwa kwa bei rahisi na maharamia wa kazi za sanaa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *