Mbunifu wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali amesema kuwa mwanamitindo Calisah hana sifa ya kuwa mwanamitindo kabisa.

Mustafa Hassanali amesema kama Calisah angekuwa mwanamitindo mwenye sifa angeshafanikiwa kwenda kwenye majukwaa ya mitindo kimataifa, lakini kwa kuwa hana sifa, hata ya hapa nyumbani ameshindwa kufanikiwa kupanda.

Mustafa ameendelea kwa kusema kwamba tasnia ya mitindo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, na kama huna nidhamu basi hakuna utakalofanikisha.

Kitendo cha mwanamitindo huyo kutolewa sifa na watu walioko kwenye tasnia yake imekuwa ni mara ya pili, ambapo awali mwanamitindo Dax Cruzz alisikika akisema Calisah hana vigezo vya kuwa mwanamitindo wa kimataifa na kwamba ataishia hapa hapa bongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *