Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameukataa mualiko wa Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa wa kushiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru jijini Harare, Jumatano iliyopita.
Kwa mujibu wa NewsDay, Mugabe alipokea mualiko rasmi kutoka Ikulu, ambapo ilitarajiwa kuwa angehudhuria kwa mara ya kwanza akiwa sio rais wa nchi hiyo.
Msemaji wa Ikulu, George Charamba amesema kuwa awali Mugabe alionesha kuwa atashiriki tukio hilo lakini hakufika kwenye viwanja hivyo.
Alisema kuwa huenda Mugabe alikuwa amechoka kwani alikuwa ametoka safari ya Mashariki ya Mbali hivi karibuni, hivyo alishauri aachwe apumzike.
Zimbabwe iliadhimisha miaka 38 ya uhuru, Aprili 18 katika jiji la Harare. Rais Emmerson Mnangagwa aliahidi kufanyika kwa uchaguzi huru na haki mwaka huu.