Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amekataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuwepo kwa wito wa kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo.

Mugabe mwenye umri wa miaka 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jeshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema.

Kwa upande wake kiongozi wa upinzani nchni humo, Morgan Tsvangirai amesema kuwa kwa manufaa ya watu wa Zimbabwe Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.

Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke wake Grace Mugabe, kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF na kuwa rais wa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa Bw. Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.

Maafisa wa Zanu PF mapema walikuwa wamesema kuwa Mugabe atasalia madarakani hadi ufanyika mkutano mkuu wa Chama mwezi Disemba wakati Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *