Mtu mmoja amaeuawa kwa kupigwa risasi na wailinzi wa Ikulu ya Kenya baada ya kujaribu kuruka ukuta na kuingia ndani ya Ikulu hiyo.
Mtu huyo asiyefahamika na mwenye umri wa makamo alidaiwa kuingia bila ruhusa kwenye maeneo yanayolindwa vikali kabla ya saa 11 jioni na alikuwa kwenye eneo la maegesho ya magari.
Maafisa wa usalama wamesema kuwa wanaamini mtu huyo aliruka uzio wa ikulu hiyo sababu haiwezekani kuingia ndani bila kupita getini ambako nako hadi uruhusiwe.
Hii ni mara ya kwanza mtu yeyote kupigwa risasi na kuuawa ndani ya viwanja vya ikulu, lakini hilo ni tukio la tatu kwa mtu kuingia bila ruhusa tangu Rais Kenyatta ahamie humo mwaka 2013.
Chanzo kimoja kimesema mtu huyo alikuwa na kisu na kingine kudai hakuwa na silaha. Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi.