Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kufuatia ufyatuaji wa risasi kwenye klabu ya usiku huko Cincinati jimbo la Ohio nchini Marekani.
Takriban watu wawili waliokuwa na silaha walitekeleza shambulizi kwa mujibu wa polisi katika jimbo.
Kapteni wa polisi Kimberly Williams alisema kuwa polisi hawana taraifa kuhusu washambuliaji hao.
Kisa hicho kinatokea chini ya mwaka baada ya Omar Mateen, kufyatua risasi kwenye klabu ya wapenzi wa jinsia moja mjini Orlando huko Florida.
Mateen aliwaua watu 49 katika kisa ya kibaya zaidi cha ufyatuaji risasi katika historia ya Marekani.