Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya basi la abiria kugonga treni leo majira ya asubuhi.
Basi hilo (T 435 DGG) lilikuwa linatoka Gongo la Mboto kwenda Mnazi Mmoja limegonga treni ya Pugu leo saa 11 alfajiri katika makutano ya reli na barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.
Katika akali hiyo majeruhi wa ajali ni 23 , wanane wapo hospitali ya Amana na waliobakia 15 wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili MOI watatu kati yao ni mahututi.
Baada ya ajali hiyo treni hiyo ya Pugu inaendelea na huduma zake kwa kufuata ratiba kama kawaida yake.
Taarifa hii imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL jijini Dar es Salaam.