Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru.

Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi baada ya kutekwa miaka miwili iliyopita.

Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.

Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.

Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao.Wasichana wa Chibok baada ya kupokewa na serikali

Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo Chibok nchini Nigeria.

Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameolewa na wapiganaji na wamepata watoto nao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *