Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amebainisha kupungua kilo saba ikiwa ni siku 7 tu zimepita toka awekewe puto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila ili kumsaidia kupunguza uzito mwilini mwake.
Msechu ameelezea mafanikio hayo kwa furaha na kuonesha shauku ya kutamani kujua miezi sita kutoka sasa atakuwa katika hali gani kwani ndio utakua muda wa kulitoa puto hilo tumboni kwake.
Amesema kuwa “Niliwekewa puto January 25 mwaka huu leo ni siku ya saba nimepunguza kilo 7 ina maana kila siku inazikwa kilo 1, Muhimbilii hii mmetisha, asante sana Mh. Rais wangu Dkt. Samia.
Ameongeza kwa kusema kuwa ‘Hii huduma umeileta Nchini kwetu hakika umekuja kunikomboa, asanteni sana Wizara ya afya kwa kuhakikisha mnajali afya zetu Watanzania, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu haki ya nani umetisha”
“Kipekeee kabisa asanteni Wataalamu wote na Madakatari kutoka Mloganzila, haki ya nani mmebadilisha maisha yangu tayari ndani ya wiki moja tu, Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili Profesa Janabi kongoleeeeeeee sanaaaaaaaa, nasema hivi hii ni wiki moja tu kilo saba je mwezi mmoja ? je miezi miwili? je mpaka nitakapolitoa mwezi wa sita?”