Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami baby amesema haoni tatizo lolote la yeye kumsifia Irene Uwoya kwa madai wana historia ndefu ya maisha yao ya nyuma kabla ya kuolewa.

Msami amefunguka hayo baada ya wawili hao kuzua ngumzo mitandaoni kwa kile kilichoonekana kuwa bado wanatamania kimapenzi japokuwa mmoja wapo amekuwa mke wa mtu kwa sasa.

Amesema kuwa “Ni kweli Uwoya anapenda ninachokifanya ndio maana ameni-post ni kweli kwani kuna kitu gani cha uongo hapo wakati amezungumza ukweli. Kama kucheza ninacheza kwa hiyo anahaki ya kusema anachotaka.

Amesema kuwa kwake kuandika mtu fulani ni mzuri sio dhambi kwasababu kwangu mimi binafsi naona kama upendo wa kumkubali mtu kama yeye alivyoona kuwa mimi ninasifa ya kuwa mchezaji bora.

Pamoja na hayo, Msami ameendelea kwa kusema “mimi namjua Uwoya tokea zamani, kwa hiyo tuna maisha yetu na historia, tunaongea na kutaniana mambo mengi,’so’ haviwezi vitu kama hivyo kuanza kupotea tu”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *