Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msamii amefunguka na kusema kuwa kwasasa hayupo tayari kuonekana katika video ya msanii yeyote kwani anataka kufanya kazi zake mwenyewe.
Msami ambaye ni dansa maarufu Bongo amesema kuwa amechukua uamuzi huo ili kuweza kufanya zaidi kazi zake binafsi ili kupeleka mbele muziki wake.
Msanii huyo amesema kuwa hawezi kuonekana kwenye video ya msanii yoyote kwa namna yoyote ile iwe kucheza au kuuza sura labda kuwe na faida kubwa sana kwake.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa kwasasa amejikita zaidi kufanya muziki wake na kazi ya uchezaji amewaachia watu wengine kwa sababu ameona umefika wakati wa kufanya hivyo ili na wengine wapate nafasi hiyo pia.
Mwanamuziki huyo ni zao la jumba la vipaji nchini THT ambapo alianza kama dansa lakini kwasasa ameingia rasmi kwenye muziki ambapo kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Mdundo’.