Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami Baby amefunguka na kusema kuwa alapata msala wa kesi ya kuua mwezi wa pili mwaka huu ambayo ilimfanya kukaa ndani kwa wiki mbili.

Mwezi wa pili nilipata matatizo kidogo, nilishutumiwa kuua. Tulienda swimming jamaa mmoja akafariki ikaonekana labda sisi tumemuwekea madawa, kilichotusadia kulikuwa na CCTV Camera

Nilivyokamatawa nilikosa dili kubwa la Milioni 10, sikuwa na wasiwasi kwa kuwa hawakuwa na ukweli wa ile kesi, nilikaa wiki mbili kituo Oyster Bay” amesema Msami Baby.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwasasa anajipanga kurudi tena kwenye game baada ya kimya chake hicho cha muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *